1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiEthiopia

Ukatili majumbani,ndoa za utotoni zaongezeka Ethiopia

16 Februari 2023

Utafiti uliofanywa na shirika la kimataifa linalohudumia watoto UNICEF umeonyesha ndoa za utotoni, ambazo ni kinyume cha sheria nchini Ethiopia, zimeongezeka kwa kiasi kikubwa

Afghanistan, Mazar-i-Sharif | Flüchtlinge beim Wasserholen
Picha: Rahmat Alizadah/Xinhua/imago

Katika mikoa minne mikubwa nchini humo imeongoza katika kipindi cha miezi sita ya kwanza mwaka 2022 ikilinganishwa na mwaka 2021.

Bisharo mwenye umri wa miaka 14 ambaye si jina lake halisi aliozwa kwa mahari ya dola 56.

Ikiwa amelazimishwa kuolewa na familia yake alikaa siku tano pekee na mume wake mpya aliyekuwa akimnyanyasa kabla ya kutoroka na kwenda kujitafutia chakula kusini mwa Ethiopia eneo ambalo linakabiliwa na ukame.

Bisharo anasema wazazi wake pamoja na wazazi wa mume wake walikubaliana kuhusu mpango huo wa ndoa, huku yeye akiwa hafahamu suala hilo.

Mwanaume huyo aliyetaka kumuoa alimfuata kabla na kumuuliza kama angependa kuolewa naye lakini yeye hakukubali ombi hilo.

Soma pia:Kampeni ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake yaanza

Bisharo anasema mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 20, anatoka ukoo mmoja na baba yake licha ya yeye kutaka kumuoa lakini tayari alikuwa na mke lakini mpango huo ulitekelezwa.

Mateso katika ndoa yakulazimishwa

Mwathirika ukatili majumbaniPicha: Bay Ismoyo/AFP/Getty Images

Bisharo anasema waliishi pamoja na mwanamume huyo kwa siku tano, huku akimpiga kila wakati  sababu alitaka kufanya mapenzi na binti huyo, lakini licha ya kuwa alikuwa akipigwa hakukubali kufanyiwa kitendo hicho.

Bisharo anasema bado anahisi maumivu mgongoni, mabegani na kichwani kutokana na unyanyasaji aliovumilia baada ya ndoa yake mapema mwezi Januari.

"Siwezi hata kulala usiku kwa sababu ya maumivu." Bisharo alisema

Aliongeza hakuweza kuvumilia ukatili huo ilimlazimu kutoroka na kukimbilia kuomba hifadhi katika nyumba ya jirani.

Bisharo anasema baadaye mume huyo alikamatwa na polisi, ambao waliomba talaka itolewe, kinyume na matakwa ya babake Bisharo.

Soma pia:Wavulana milioni 115 duniani kote waliingia ndoa za utotoni

Lakini haikuwa rahisi kwa Bisharo kwani baba yake alimwambia ukikubali kuachana mimi sio baba yako tena na huwezi kuniita baba.

Kutengwa na familia baada ya talaka

Bisharo anasema ndugu zake hawakuwa na msaada wowote isipokuwa mama yake ambaye alielewa changamoto anazopitia lakini hakuweza kumsaidia kwa kuwa alikuwa namuogapa baba yangu.

Ukatili wa kijinsia, tunapambana nao vipi?

02:44

This browser does not support the video element.

Bisharo, alitafuta usaidizi katika kliniki mpya iliyofunguliwa kwa ajili ya manusura wa unyanyasaji wa kijinsia katika hospitali moja mjini Gode nchini Ethiopia ambayo husaidia wanawake na wasichana kuwapatia mahitaji.

Ni miongoni mwa maeneo ambayo yamekumbwa na ukame mkali katika Pembe ya Afrika ambayo yamewaacha mamilioni ya watu wakiwa na njaa na umaskini katika hali ya ukame zaidi katika kipindi cha miaka 40.

Madaktari na wafanyakazi katika jamii hiyo wanasema ongezeko la ndoa za kulazimishwa na unyanyasaji wa kijinsia unasababishwa na ukame wa muda mrefu katika eneo hilo ambao umekuwa ukisababisha madhara mengi.

Fahad Hassan ni daktari katika kliniki hiyo  anasema tangu kufunguliwa kwa jengo hili dogo mwezi Novemba mwaka uliopita.

Soma pia:Nigeria: Ndoa za utotoni bado tatizo kubwa

Limepokea manusura wanane wa ubakaji, wakiwemo wanawake wanne na wasichana wanaotoroka unyanyasaji wa kijinsia majumbani.

"Ukame ndio chanzo cha visa hivyo vingi" alisema Dkt Fahadi.

Aliongeza mara nyingi hutokea katika kambi za muda za Abaqoro zilizowekwa kwa ajili ya kuhifadhi watu waliolazimika kukimbia ukame huku kambi hizo zikiwa zinawaweka wanawake na wasichana katika hatari.

Kambi zafichua dhuluma zaidi

Dkt Fahad anasema msichana mwenye umri wa miaka saba aliletwa katika zahanati hiyo baada ya kubakwa katika kambi ya Abaqoro karibu na wilaya ya jirani.

Sahra Haji Mohammed ni moja ya mfanyakazi wa kijamii anasema mashambulizi dhidi ya wanawake yanatokea wakati wakitoka kambini kwenda kununua mahitaji au kwenda kutafuta maji, na umasikini pia umekuwa sababu inayochangia unyanyasaji katika ndoa.

Manusura wa ukatili majumbaniPicha: Evelyn Kpadeh/DW

Dkt Fahad anasema waathirika wengi wa unyanyasaji wa kijinsia katika eneo hili wanaamua kukaa kimya wakihofia kunyanyapaliwa na jamii zao za kitamaduni.

Hata sisi wenyewe tunatoka kwenye jamii hizo tunajua kesi ambazo haziji hapa lakini ziko majumbani mwao na wanajaribu kujificha lakini tunajaribu kuzungumza nao kuwa kituo hiki ni maalumu kwa ajili ya kuwasaidia.

Soma pia:Somalia huenda ikahalalisha ndoa za utotoni

Dkt Fahadi anasema mbali na unyanyasaji wa kijinsia, wengi katika jamii hawaoni uhalifu huu dhidi ya wanawake kuwa ni makosa na yanayohitaji kushughulikiwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW