1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UKIMWI wasambaa Afrika:

26 Novemba 2003
PARIS: Ukimwi unasambaa kusini mwa Afrika. Hii ni ripoti ya mwaka ya Mpango wa Ukimwi wa Umoja wa Mataifa UNAIDS ambayo imechapishwa mjini Paris. Thuluthi moja ya wagonjwa millioni 40 duniani wenye virusi vya ukimwi, wanaishi katika nchi za eneo hilo. Kwa mujibu wa shirika UNAIDS hakuna nchi yo yote ya kiafrika iliyofanikisha kampeni yake ya kupambana na ukimwi, isipokuwa Uganda na Senegal. Ulimwengu umekabiliwa na uamuzi, - unaonya mpango huo wa Umoja wa Mataifa. Kila hatua inapaswa kuchukuliwa kuushinda ukimwi. Mwaka huu kote duniani walifariki wagonjwa millioni tatu wa ukimwi, na millioni tano wameambukizwa virusi.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW