1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Shughuli zasitishwa Ukingo wa Maghabiri kupinga hujuma Gaza

11 Desemba 2023

Shughuli zimesitishwa kote Ukingo wa Magharibi katika Mamlaka ya Wapalestina kama hatua ya kupinga vita vinavyoendelea Ukanda wa Gaza.

Athari za mashambulizi ya Israel huko Ukingo wa Magharibi
Kama ilivyo Ukanda wa Gaza, Israel imekuwa pia ikilishambulia eneo la Ukingo wa Magharibi.Picha: Majdi Mohammed/AP/picture alliance

Shughuli za kibiashara, shule na ofisi za serikali zimesimama katika eneo hilo leo Jumatatu, huku vyombo vya habari vikiripoti kwamba usafiri wa umma, mabenki na vyuo vikuu pia wamejiunga na mgomo huo unaolenga kuonesha mshikamano na mwito wa kutaka vita visitihwe Gaza.

Ama kwa upande mwingine, wanajeshi wa Israel wameshambulizi eneo la mpakani kujibu maroketi yaliyofyetuliwa kutoka Lebanon.

Jeshi la la Israel limesema limeyaharibu maroketi sita yaliyorushwa kutoka Lebanon huku ripoti za kituo cha utangazaji cha televisheni cha Hezbollah,Al Manar kikiripoti kwamba vijiji kadhaa katika eneo la mpakani vimeshambuliwa na Israel.

Nchini Israel kwenyewe gazeti la The Haaretz limeripoti kwamba mamia ya Wapalestina waliokamatwa hadi sasa ni asilimia kiasi 10 hadi 15 pekee ndio wanachama wa kundi la wanamgambo la Hamas.

Jeshi la Israel hata hivyo limesema sheria ya kimataifa imezingatiwa katika hatua za kuwakamata Wapalestina.