Ukoloni ni mada iliyopuuzwa katika historia ya Ujerumani, ingawa kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia, yaliyokuwa makoloni ya Ujerumani barani Afrika yalikuwa ya tatu kwa ukubwa duniani kote. Inakuwaje Wajerumani wana ufahamu mdogo kuhusu ukoloni wao wa zamani na matokeo ya ukosefu wa ufahamu huo ni yapi?