1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukombozi wa kambi ya Auschwitz wakumbukwa

Oumilkher Hamidou27 Januari 2012

Ulimwengu unaadhimisha miaka 67 ya kukombolewa kambi ya maangamizi ya wanazi ya Auschwitz.Mmojawapo wa waliosalimika muandishi sanifu Marcel Reich-Ranicki amehutubia bunge la shirikisho hii leo.

Der Literaturkritiker und Überlebenden des Holocaust, Marcel Reich-Ranicki, spricht am Freitag (27.01.2012) im Bundestag in Berlin. Zum 67. Jahrestag der Befreiung des Konzentrationslagers Auschwitz hält Reich-Ranicki die Gedenkrede vor dem Bundestag. Foto: Hannibal dpa/lbn
Bunge la shirikisho laadhimisha miaka 67 ya kukombolewa AuschwitzPicha: picture-alliance/dpa

Rais wa shirikisho Christian Wulff,kansela Angela Merkel na mwenyekiti wa sasa wa baraza la wawakilishi wa majimbo-Bundesrat,Horst Seehofer ni miongoni mwa wanaohudhuria kikao hicho maalum kuwakumbuka wahanga wa kambi ya mateso na maangamizi ya wanazi- Auschwitz iliyokombolewa na vikosi vya Soviet Union January 27 mwaka 1945 .

Mwandishi sanifu Marcel Reich-Ranicki ,mwenye umri wa miaka 91 na ambae ni miongoni mwa waliosalimika na mateso na maangamizi katika kambi hiyo ya karibu na mji mkuu wa Poland Warsau,amekumbusha jinsi walivyokuwa wameandamwa na jinsi wanazi walivyoandaa mauwaji ya halaiki.

Mwanadishi sanifu Marcel Reich-Ranicki (watatu kutoka kushoto) na spika wa bunge la shirikisho Norbert Lammert (kulia)Picha: dapd

Katibu mkuu wa baraza kuu la wayahudi nchini Ujerumani Stephan Kramer amesema maadhimisho haya yamelengwa zaidi kuzifikia nyoyo za kizazi kipya ambacho hakijashuhudia madhila yaliyotokea.

Spika wa bunge la shirikisho Norbert Lammert ameitolea mwito jamii iwe macho zaidi dhidi ya makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia na hisia za chuki dhidi ya wayahudi."Linabidi liwe lengo na jukumu la kila mmoja,kuhakikisha kwamba watu nchini Ujerumani wanajivunia uhuru ,usawa na kuishi bila ya wasiwasi" amesema spika huyo wa bunge wa kutoka chama cha Christian Democratic Union.Ameutaja uchunguzi uliochapishwa hivi karibuni na kuonyesha kwamba asili mia 20 ya wajerumani kichini chini wanahisia za chuki dhidi ya wayahudi kuwa si jambo linalokubalika.

"Kufichuliwa hivi karibuni visa kadhaa vya mauwaji yaliyofanywa na wafuasi wa siasa kali ya mrengo wa kulia ni ushahidi kamili kwamba watu wanalazimika kuwa macho zaidi na kuwajibika zaidi dhidi ya makundi ya siasa kali za mremngo wa kulia" amesisitiza spika wa bunge la shirikisho Nobert Lammert.

Makumbusho ya kambi ya mateso ya Auschwitz

Kambi ya Auschwitz inaangaliwa kama kitambulisho cha ukatili uliofanywa na utawala wa wanazi pamaoja na mauwaji ya halaiki ya mamilioni ya wayahudi kati ya mwaka 1939 na 1945.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/epd/dapd/dpa/afp

Mhariri: Abdul-Rahman,Mohammed

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi