Ukosefu wa ajira wapanda kwa 4% Uingereza
11 Julai 2023Matangazo
Ukosefu huo wa ajira unatokea wakati Uingereza inakabiliwa na mfumuko wa bei za bidhaa.
Ofisi ya Takwimu ya nchi hiyo (ONS) imesema kiwango cha ukosefu wa ajira kimeongezeka kutoka 3.8% katika miezi mitatu ya kuelekea mwisho wa mwezi Aprili.
Licha ya kiwango hicho kuongezeka, Waziri wa Fedha Jeremy Hunt amesema soko la ajira la Uingereza liko imara na kwamba ukosefu wa huo ajira uko chini tofauti na miaka ya awali.
Ofisi ya ONS imeeleza kuwa mishahara bila ya kujumuisha marupurupu imeongezeka katika viwango vya kuvunja rekodi.
Mfumuko wa bei Uingereza umepungua katika miezi ya hivi karibuni, japo viwango bado vinakaribia asilimia tisa.