Ukosefu wa madawa waripotiwa wilayani Rubero
19 Mei 2025
Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kumekuwa na ripoti nyingi za ukosefu wa madawa muhimu katika vituo vya afya kwenye vijiji vya mangurujipa na Biena wilayani Lubero. Hali hii inatokana na waasi wa ADF wenye asili ya Uganda kuimarisha shughuli zao, na hivyo kuathiri usafirishaji wa bidhaa muhimu, ikiwemo madawa, kama anavyoeleza KAYITSUPA Gerlas mwanaharakati wa asasi zakiraia wilayani humo.
Insert : "kuna baadhi vituo vya afya ambavyo vimesitisha shughuli zake kutokana na uhaba wa madawa na vituo vingi ni vile vilivyo porwa na waasi wa ADF na vingine viliunguzwa. Kwa hiyo wakazi wamekosa pia pesa zakununua dawa nakusababisha vituo hivyo kushindwa tena kufanya kazi."
Mbali na usalama mdogo unaoshuhudiwa kwenye eneo hilo ufukara wa wakazi pamoja na uchakavu wa miundombinu ya barabara ndio sababu kubwa ya wagonjwa wengi kufariki kabla yakufika kwenye vituo vya Afya jambo ambalo linaongeza uwezekano wa hadi watu 15 na zaidi wanaofariki kila siku ameeleza afisa huyo.
Vijiji vya Biena na Mangurujipa ndivyo vilivyoathirika zaidi
"kila siku tunaorodhesha vifo vya watu zaidi ya 15 kwenye vijiji vya mangurujipa na Biena ,baadhi ya wagonjwa wanakosa pesa kwa ajili ya matibabu na wengine huwasili hospitalini wakiwa mahututi ".
Vijiji vya Biena na Mangurujipa vilivyopo magharibi mwa mji wa Butembo, ndivyo vimeathirika pakubwa na uhaba huo wa madawa huku baadhi ya vituo vya afya vikilazimika kukatiza huduma za matibabu kwa wananchi wanaoitaka serikali kuingilia kati haraka iwezekanavyo ili kulitatua tatizo hilo.
"tunaisihi serikali ili wananchi wa vijiji vya mangurujipa wapate usalama na iwapo kuna wadhamini wengine watusaidie na madawa sababu hospitali nyingi zimefunga milango ".
Uhaba huo wa madawa hata hivyo, umekua ni kitishio kikubwa kwa maelfu wa raia wanaohangaika sababu ya ukosefu wa usalama kwenye wilaya ya Lubero ambayo ni ya pili kuwa chini ya udhibiti wa kundi hilo la wapiganaji wa ADF tangu mwanzoni mwa mwezi wa juni mwaka uliopita.