1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SafariKenya

Ukosefu wa vipuri wavuruga safari za shirika la ndege Kenya

11 Desemba 2023

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, limewaarifu wateja wake kujiandaa kushuhudia mabadiliko ya ratiba ya safari zake za ndege katika kipindi cha msimu wa sikukuu ya Krismasi kutokana na ukosefu wa vipuri.

Kushoto ni bango la kampuni ya ndege ya Kenya, Kenya Airways.
Mbali ya kuwa moja ya mashirika makubwa ya ndege barani Afrika, Kenya Airways imekuwa ikipitia misukosuko mingi miaka ya karibuni.Picha: Simon Maina/AFP

Kwa mujibu wa shirika hilo ukosefu huo wa vipuri  ambao ni tatizo katika soko la usambazaji dunia nzima, utasababisha ratiba za safari za ndege kuvurugika kwa kipindi cha kiasi  wiki mbili.

Ndege za shirika hilo zitalazimika kuchukua muda mrefu kusubiri kufanyiwa matengenezo kabla ya kuanza safari zake.

Shirika hilo  ambalo ni moja ya mashirika makubwa ya ndege barani Afrika limesema matatizo hayo kwa mara ya kwanza, yalianza kushuhudiwa mwezi Januari mwaka huu.

Wakati huo lilieleza kwamba yalichangiwa na vita vya Ukraine kutokana na soko la usambazaji vipuri vya ndege  la Urusi lilikuwa na changamoto.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW