1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine ilitibua mipango ya Urusi, Poland

25 Julai 2024

Idara ya Usalama nchini Ukraine imesema hii leo kwamba imezima mpango wa Urusi wa kushambulia kwa moto majengo yenye maduka kuanzia Poland hadi mataifa ya Baltiki na ndani ya mipaka yake.

Belgien | EU Gipfel Wolodymyr Selenskyj
Picha: Johanna Geron/REUTERS

Idara hiyo, SBU imesema watu 19 wanashikiliwa miongoni mwa 37 baada ya upekuzi kwenye mikoa minne ya Ukraine, na maafisa wa usalama pia wamekamata pasi bandia za kusafiria pamoja na leseni za kuendesha gari.

Polisi nchini Ukraine pia imethibitisha kamatakamata hiyo, na kusema kiongozi wa operesheni hiyo alikamatwa katika jimbo la Ivano-Frankivsk, magharibi mwa Ukraine.

Mashambulizi hayo ambayo yangehusisha kuchoma moto vituo vya mafuta, maduka ya dawa na masoko yalipangwa kufanywa na raia wa Ukraine chini ya maagizo ya Moscow ili kuidhoofisha Ukraine na hata msaada kutoka magharibi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW