1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Ukraine imedungua makombora zaidi ya 30 ya Urusi

2 Juni 2023

China iko tayari kuzingatia kutuma ujumbe mwingine barani Ulaya kwa mazungumzo juu ya kutatua mgogoro wa Ukraine.

Ukraine | Mobiles Flugabwehrsystem Kiew
Picha: Oleksandra Indyukhova/DW

Haya yanajiri wakati Jeshi la Ukraine mjini Kyiv limesema kwamba limedungua zaidi ya makombora 30 ya Urusi pamoja na droni, usiku wa kuamkia leo.

Soma pia;  Urusi yafanya mashambulizi mapya ya anga mjini Kiev

Akizungumza na vyombo vya habari mjumbe wa masuala ya umoja wa ulaya na Urusi Li Hui amesema kwamba safari yake ya Ulaya mwezi uliopita, ikiwa ni ziara ya kwanza ya kutafuta suluhu la kisiasa juu ya mgogoro huo haiwezi kusababisha matokeo yoyote ya haraka na kwamba walihisi kuna pengo kubwa kati ya pande zinazozozana.

Mnamo Mei, Li alikamilisha ziara ya siku 12  katika miji ya Kyiv, Warsaw, Paris, Berlin, Brussels na Moscow katika nia ya kutafuta msingi wa pamoja katika vita vya Urusi na Ukraine.

Katika uwanja wa mapambano raia wawili wameuwawa leo Ijumaa kutokana na mashambulizi ya makombora katika eneo laBelgorod nchini Urusi, linalopakana na Ukraine.

Gavana wa Belgorod Vyacheslav Gladkov amesema kwamba vikosi vya Ukraine vilifyatua risasi katika barabara ya kijiji cha Maslova Pristan, katika wilaya ya Shebekino ambayo imeathiriwa zaidi na mashambulizi ya hivi majuzi.

Soma pia;Eneo la mpakani kati ya Urusi na Ukraine laendelea kuwa tete 

Kupitia mtandao wa Telegram mamlaka ya jeshi la Ukraine, imesema Urusi ilifyetuwa makombora ya kasi kwa kutumia droni na ndege za kivita yakilenga maeneo tofauti lakini yaligunduliwa na kuharibiwa yakiwa kwenye anga ya mji mkuu Kyiv na jeshi la ulinzi.

Maeneo ya kujikinga 

Eneo la kujikinga na mashambulizi ya angaPicha: Evgeniy Maloletka/AP/picture alliance

Huku haya yakijiri Rais Volodymyr Zelenskyy hapo jana alitoa wito kwa wananchi wa Ukraine kuweka wazi makazi ya kujikinga na mashambulizi ya anga muda wote baada ya mwanamke mmoja kuuwawa katika mashambulizi alipokuwa akingoja kuingia kwenye eneo la kujikinga.

Soma pia: Viongozi wa Ulaya waungana dhidi ya Urusi mkutano wa Maldova

Rais Zelenskyy ameongezea kusema kwamba serikali yake inajiandaa kwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya kujihami ya NATO mwezi ujao huko Vilnius na anatafanya kila iwezekanalo kuendeleza ujio wa Ukraine katika Umoja wa Ulaya.

"Tunatayarisha maamuzi mapya ya ulinzi wa Ukraine, ikiwa ni pamoja na ulinzi wa anga, usafiri wa anga, na maendeleo yetu ya ardhini. Tunatayarisha maudhui halisi ya kisiasa kwa ajili ya mkutano wa kilele wa NATO huko Vilnius. Tunatayarisha kifurushi cha dhamana ya usalama kwa nchi. Tunafanya kila kitu ili kuleta uamuzi wa kisiasa wa Umoja wa Ulaya kuhusu uanachama wa Ukraine karibu.

Maafisa wa Urusi wameripoti mashambulizi zaidi ya mpakani kutoka Ukraine na kusema ndege mbili za masafa marefu zilishambulia miundombinu ya mafuta na nishati upande wa kaskazini lakini hakuna majeruhi walioripotiwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW