Ukraine imepokea mkopo kutoka kwa nchi za Umoja wa Ulaya
21 Desemba 2023Matangazo
Wanachama wa nchi za Umoja wa Ulaya walikubaliana mwezi Desemba mwaka jana juu ya msaada jumla wa euro bilioni 18 kwa Ukraine.
Haijulikani jinsi msaada wa Umoja wa Ulaya kwa Ukraine utakavyoendelea mwaka ujao, baada ya mpango mpya wa msaada wa thamani ya euro bilioni 50 kupingwa ba Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán wiki iliyopita.
Hungary yazuia msaada wa mabilioni ya dola kwa Ukraine
Mkutano maalum wa kilele wa Umoja wa Ulaya kuhusu kuendelea kuisaidia Ukraine umepangiwa kufanyika tarehe mosi mwezi Februari mwaka ujao.
Ukraine ina hadi miaka 35 ya kulipa fedha hizo, kuanzia mwaka 2033. Gharama za riba zitalipwa na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.