1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine inaandaa kesi kadhaa za uhalifu wa kivita

14 Mei 2022

Timu ya uchunguzi wa uhalifu wa kivita ya Ukraine imesema iko tayari kuwashitaki washukiwa wengine 41 baada ya kesi ya kwanza ya mwanajeshi wa Urusi kuanza kusikilizwa mjini Kyiv

Ukraine Krieg mögliche Kriegsverbrechen in Butscha
Picha: Zohra Bensemra/REUTERS

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Ukraine Iryna Venediktova amesema jana Ijumaa(13.04.2022) imewasilisha kesi 41 mahakamani dhidi ya wanajeshi wa Urusi. Amesema kesi zote zinaongozwa na sheria ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu vbya Ukraine.

Katika taarifa yake kupitia televisheni ya umma ya Ukraine, Venediktova amesema miongoni mwa ushahidi walionao kuhusu kesi hizo ni pamoja na kuyashambulia kwa mabomu maeneo ya makazi ya watu, kuuwa watu, kuwabaka na wizi. Hata hivyo haijawa wazi ni watuhumiwa wangani wanaweza kuhukumiwa pasipo kuwepo mahakamani.

Jana Ijumaa mjini Kyiv ilikuwa siku mwanzo kabisa kupiandishwa kizimbani kwa mwanajeshi wa Urusi, kijana wa umri wa miaka 21 kwa tuhuma ya kumuua raia alikuwa hana silaha katika siku za mwanzo za vita vya Ukraine.Venediktova alisema kuwa washukiwa wawili zaidi, ambao wanashikiliwa nchini Ukraine, huenda wakapanda kizimbani wiki ijayo.

Mmoja ameuwawa na wengine 11 wamejeruhiwa Donetsk.

Kitengo cha dharura cha Urusi kinasafisha mabaki DonetskPicha: Peter Kovalev/TASS/dpa/picture alliance

Makombora ya Urisi yamemua aia mmoja na watu kumi na wawili zaidi walijeruhiwa katika mkoa wa mashariki mwa Ukraine wa Donetsk wa Ukraine. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa gavana wa eneo hilo.

Mkoa wa Donetsk, ni mmoja kati ya miwili ambayo inaunda eneo la Donbas, ukanda ambao umeshuhudia mapigano makali katika majuma ya hivi karibuni, kutokana na serikali ya Urusi kuzidisha mashambulizi yake kwa shabaha ya kudhibiti eneo la kiviwanda huko mashariki mwa Ukraine.

Urusi imetangaza kuikatia umeme Finland

Urusi imetangaza kusitisha usambazaji wa umeme nchini Finland katika siku hizi za mwisho wa juma katika kipindi hiki ambacho mvutano unaongezeka kutokana na jitihada za serikali ya Helsinki kujiunga na Umoja wa Kujihami wa NATO, na uvamizi wa kijeshi wa serikali ya Urusi kwa Ukraine.

Soma zaidi:Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema nchi yake haitalitambua jimbo la Crimea kuwa ni sehemu ya Urusi.

Shirika  la nishati la Urusi Inter Rao limesema imelazimika kusitisha usafirishaji wa mafuta kuanzia Mei 14, kutoka na kampuni yake tanzu RAO Nordiv kushindwa malipo ya kulipia umemea kutoka Urusi.

Hatua hiyo inafuatia baada ya Alhamisi, Finland kusema itaomba kujiunga na muungano wa ulinzi wa kijeshi wa NATO unaongozwa na Marekani na Sweden pia kutarajiwa kufuata mkondo huo wa jirani yake mapema Jumatatu.

Vyanzo: AP/AFP/DW

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW