Ursula: Ukraine itaamuwa juu ya mahusiano ya China na EU
30 Machi 2023![Ursula von der Leyen / Rede 30.03.2023](https://static.dw.com/image/65182161_800.webp)
Matangazo
Hata hivyo amesema kuwa Ulaya haitaki kutengana na China. Akizungumza mjini Brussels, von der Leyen amesema ni wazi kuwa china, chini ya Xi inaanza kuwa kandamizi zaidi ndani ya nchi na yenye uthubutu zaidi nje ya nchi.
Rais huyo wa Halmashauri Kuu ya Ulaya ataandamana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenda Beijing wiki ijayo huku viongozi wa Ulaya wakilenga kufanya mashauriano na Rais wa China Xi Jinping.