Ukraine itahitaji msaada wa Ulaya kwa miaka 2 au 3 zaidi
28 Oktoba 2025
Zelensky ameyasema haya huku akikiri kwamba vikosi vya Urusi vimepiga hatua mashariki mwa Ukraine katika mji wa Pokrovsk, ambao wamekuwa wakijaribu kuuteka kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
"Nilizungumza na jeshi letu na wanalitazama kwa karibu eneo la Pokrovsk na maeneo ya karibu. Huko ndiko Urusi ilipoweka sehemu kubwa ya vikosi vyake na ndiko kwenye mashambulizi zaidi. Mapambano yanaendelea katika mji huo pia kwa kuwa Pokrovsk ndio lengo lao kubwa. Matokeo yoyote yatakayopatikana na vikosi vyetu ni kutokana na Ukraine nzima, kwa ulinzi jumla wa taifa letu," alisema Zelenskiy.
Zelensky vile vile amemtaka Rais wa Marekani Donald Trump, kumuwekea shinikizo kiongozi wa China Xi Jinping kuacha kuiunga mkono Urusi, wakati viongozi hao watakapokutana baadae wiki hii.