1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine kuimarisha uhusiano na bara la Afrika

3 Januari 2023

Uhusiano wa karibu kati ya nchi za Afrika na Ukraine unatoa fursa pana kwa pande zote. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitangaza kuwa balozi mpya zitafunguliwa katika bara la Afrika mnamo mwaka 2023.

Ukraine Weizen l Erster internationaler Gipfel zur Ernährungssicherheit in Kiew l Präsident Selenskyi
Picha: Ukrainian Presidency via ABACA/picture alliance

Katika hotuba yake mapema mwezi Desemba, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema wanaanzisha upya uhusiano na mataifa kadhaa ya Afrika na kwamba mwaka huu lazima waimarishe suala hilo. Mataifa kumi tayari yamefahamika ambako balozi mpya za Ukraine barani Afrika zitafunguliwa.

Mwezi Oktoba mwaka jana, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alifanya ziara katika nchi kadhaa za Afrika katika juhudi za kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia. Alisitisha ziara yake baada ya Urusi kufanya mfululizo wa mashambulizi makubwa ya makombora katika miji ya Ukraine kwa wakati huo.

Dmytro Kuleba, Waziri wa Mambo ya Nje wa UkrainePicha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi, Ukraine imekuwa ikijaribu kutafuta uungwaji mkono barani Afrika, huku ushawishi wa Urusi katika bara zima ukiendelea kuimarika.

Kuanza na nchini ya Ghana

Ingawa Zelensky hakutaja majina ya nchi ambazo balozi hizo zitafunguliwa, Maksym Subkh, Mwakilishi Maalum wa Ukraine katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika alikiambia chombo cha habari cha Ukraine "zn.ua" kwamba msisitizo utakuwa kwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Soma zaidi: Ukraine yataka kuungwa mkono na Afrika katika vita na Urusi

Zaidi ya hayo, Subkh alisema baada ya ziara ya Kuleba nchini Ghana kwamba uamuzi ulifanywa kuanzisha Ubalozi wa Ukraine katika nchi hiyo na ambao utafunguliwa katika miezi ijayo. Kwa sasa, hakuna nchi nyingine ambayo imebainishwa.

Aidha Subkh aliongeza kuwa Ukraine ilikuwa pia ikifanya kazi ya kuteua mabalozi katika nchi zote za Afrika ambako haikuwa na wawakilishi wa kidiplomasia.

Muda muafaka?

Wapiga ngoma za asili wa GhanaPicha: Ernest Ankomah

Oleh Belokolos, mwanadiplomasia wa zamani wa Ukraine na mchambuzi wa mashauriano ya kigeni, aliiambia DW kutoka mjini Kyiv kwamba uwepo wenye nguvu wa Ukraine barani Afrika ulikuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu.

Soma zaidi:AU yapongeza makubaliano kati ya Urusi na Ukraine yanayoruhusu tena usafirishaji nje wa nafaka kutoka kwenye bandari za Ukraine. 

Belokolos amesema waUkraine wanaelewa umuhimu wa bara la Afrika na kwamba wana amini wanao uwezo wa kupanua ushirikiano wao na nchi za hizo lakini bado ana wasiwasi kuhusu jinsi balozi hizo mpya zinavyoweza kufanya kazi haraka.

Kukuza uhusiano wa kiuchumi

Rais wa Ukraine, Volodymyr ZelenskyPicha: AFP/Getty Images

Kulingana na taarifa ya Rais Zelensky, Ukraine haivutiwi tu na kufungua balozi za uwakilishi wa kidiplomasia barani Afrika lakini pia inalenga pia kuimarisha baadhi ya uhusiano wa kibiashara.

Belokolos amebaini kwamba Ukraine ina nafasi kubwa ya ushirikiano kuanzia kwenye sekta ya kilimo hadi kwenye baadhi ya bidhaa za chakula. Hata hivyo amesisitiza kwamba kupata uungwaji zaidi kutoka kwa nchi za Afrika katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi, kutasaidia zaidi ushirikiano huu wa kijamii na kiuchumi.

Umoja wenye nguvu

Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Pavel Bednyakov/Kremlin/REUTERS

Dokta Boni Yao Gebe, mchambuzi wa masuala ya Afrika na mtafiti mwenza katika Kituo cha Masuala ya Kimataifa na Diplomasia cha Chuo Kikuu cha Ghana, wakati huo huo anaamini kwamba mataifa ya Afrika labda yabadili mfumo wao yanapoingia katika masuala ya ushirikiano na mataifa ya Magharibi. Anasema badala ya kila nchi kujadiliana kibinafsi, mataifa ya Afrika yangefaa kuwa na umoja ili kuingia mikataba ya ushirikiano, na kwamba hilo lingekuwa na manufaa zaidi kwa bara la Afrika.

Soma zaidi: Wataalamu wa siasa Afrika na Ulaya wakutana Berlin

Urusi ina balozi zaidi ya 40 katika bara hilo na imewekeza mno katika baadhi ya nchi. Hii imefanya iwe vigumu kwa baadhi ya nchi za Kiafrika kulaani vikali jukumu la Urusi katika vita vya sasa nchini Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW