Ukraine kuwaomba washirika wake ufadhili wa dola bilioni 20
12 Juni 2026
Ombi hilo litawasilishwa Alhamisi ijayo katika mkutano wa Kundi la Msaada wa Ulinzi kwa Ukraine, muungano wa zaidi ya nchi 50 unaojulikana pia kama Kundi la Ramstein, ambapo washirika hupanga na kuratibu msaada wa kifedha na kijeshi kwa Ukraine .
Kwa mujibu wa chanzo hicho, baadhi ya washirika wataombwa kuchangia kati ya dola bilioni 2 hadi 6 kila mmoja ili kufikia lengo la dola bilioni 20, ama kwa mfumo wa misaada au mikopo.
Wakati huo huo, jeshi la Ukraine lilisema leo kuwa limefanya mashambulizi ya usiku kucha dhidi ya viwanda viwili vya kusafisha mafuta katika eneo la Tatarstan nchini Urusi.
Makao Makuu ya Jeshi hilo yameeleza kuwa mashambulizi hayo ni sehemu ya operesheni zake za kulenga miundombinu ya nishati inayosaidia juhudi za kijeshi za Urusi katika vita vinavyoendelea kati ya nchi hizo mbili.