1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine kuwasilisha 'mpango wa ushindi' kwa Washirika wake

Saleh Mwanamilongo
5 Oktoba 2024

Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky amesema leo kwamba nchi yake itawasilisha ´mpango wa ushindi wa vita´ katika mkutano wa kawaida wa washirika wake huko Ramstein in Ujerumani.

Seikali ya Ukraine kuwasilisha 'mpango wa ushindi' kwenye mkutano wa Washirika utakaofanyika Ujerumani
Seikali ya Ukraine kuwasilisha 'mpango wa ushindi' kwenye mkutano wa Washirika utakaofanyika UjerumaniPicha: president.gov.ua/en

Kwenye ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wake wa Telegram, siku ya Jumamosi, Zelensky amesema mpango huo utaelezea hatua maalum na za wazi za kukomesha vita nchini Ukraine. Mkutano huo wa mjini Ramstein unapangwa kufanyika Oktoba 12.

Wakati huohuo, Mwendesha mashtaka wa Urusi ameomba kifungo cha miaka saba jela kwa Mmarekani ambaye Urusi inamtuhumu kufanya kazi kama mamluki wa Ukraine. Stephen Hubbard, mwenye umri wa miaka 72, anatuhumiwa kuajiriwa na Ukraine kama mamluki dhidi ya Urusi.

Alikamatwa na vikosi vya Urusi huko Izyum mnamo Aprili 2022 , na anakabiliwa na kifungo cha miaka saba hadi 15 ikiwa atakutwa na hatia.