1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine na EU kukutana kujadili msaada zaidi wa kifedha

3 Januari 2023

Rais Volodymyr Zelenskiy amesema Ukraine na Umoja wa Ulaya zitafanya mkutano wa kilele Februari 3 kujadili msaada wa kifedha na kijeshi.

Rais Zelensky na Rais wa Almashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen jijini Kyiv
Rais Zelensky na Rais wa Almashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen jijini KyivPicha: Sergei Supinsky/AFP/Getty Images

Zelenskiy alijadili maelezo ya kina ya mkutano huo wa ngazi ya juu na rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, katika simu yake ya kwanza ya mwaka, imesema ofisi yake katika taarifa.

Hata hivyo Msemaji wa rais wa Baraza la Ulaya Charlse Michel, hakuweza kuthibitisha hii leo kwamba mkutano huo wa kilele wa pamoja utafanyika katika mji mkuu wa Ukraine.

Lakini alisema kwamba, kanda hiyo itawakilishwa kwenye mkutano huo na Michel na von der Leyen, na siyo na viongozi mbalimbali wa mataifa ya Umoja wa Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW