1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine na Marekani kujadili kuhusu ulinzi

13 Oktoba 2025

Maafisa wa ngazi za juu wa Ukraine na Marekani watajadili kuhusu ulinzi wakati Urusi imeongeza mashambulizi dhidi ya miundo mbinu ya nishati ya Ukraine

Viongozi wa Ukraine wamekuwa wakitafuta msaada wa kijeshi kwa washirika wao wa nchi za Magharibi
Viongozi wa Ukraine wamekuwa wakitafuta msaada wa kijeshi kwa washirika wao wa nchi za MagharibiPicha: Ukrainian Presidential Press Service/REUTERS

Maafisa wa ngazi za juu wa Ukraine wameelekea Washington kwa ajili ya kushiriki mkutano pamoja na maafisa wa Marekani kuhusu ulinzi.

Hayo yameelezwa leo na ofisi ya rais Volodymyr Zelensky katika wakati ambapo Urusi imezidisha mashambulizi yake dhidi ya miundo mbinu ya nishati ya Ukraine huku Marekani ikipima uwezekano wa kuipelekea Ukraine makombora ya kisasa ya masafa marefu.

Timu ya maafisa wa Ukraine inayoongozwa na waziri mkuu Yulia Svyrydenko itajadili suala la kuimarishwa kwa mifumo ya ulinzi wa anga ya nchi hiyo pamoja na uwezo wake wa silaha, lakini pia mifumo yake ya nishati kabla ya kipindi cha baridi kali.

Wakati huohuo Urusi imesema hivi leo kwamba hakuna mpango wowote ulioandaliwa wa kufanyika mazungumzo kwa njia ya simu kati ya rais Vladmir Putin,na Donald Trump baada ya kiongozi huyo wa Marekani kuonya kwamba ataipelekea Ukraine makombora ya Tomahawk.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW