1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine na Poland kuongeza ushirikiano, asema Zelensky

23 Desemba 2023

Ukraine na jirani yake Poland, ambayo imeshuhudia hivi karibuni mabadiliko ya serikali, zinatazamiwa kuimarisha ushirikiano wao, hasa katika sekta ya ulinzi

Screenshot X | Präsident Wolodymyr Selenskyj bedankt sich bei zwei polnischen freiwilligen Helfern
Picha: twitter.com/ZelenskyyUa

Ukraine na jirani yake Poland, ambayo imeshuhudia hivi karibuni mabadiliko ya serikali, zinatazamiwa kuimarisha ushirikiano wao, hasa katika sekta ya ulinzi. Hayo ni kulingana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Soma pia: Zelensky ataka raia wa Ukraine wapambane kuilinda nchi

Wakati wa mkutano na Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Poland Radoslaw Sikorski, ambaye alikuwa Kiev jana Ijumaa katika ziara yake ya kwanzanje ya nchi, wanasiasa hao wawili walijadili kile kilichoelezwa kuwa ni fursa muhimu za kuimarisha ushirikiano - kazi ambayo itayaboresha mataifa hayo mawili. Hata kabla ya mabadiliko ya serikali mjini Warsaw, Poland ilizingatiwa kuwa mmoja wa waungaji mkono dhabiti wa Ukraine.

Nchi hiyo tayari imempa jirani yake vifaru na ndege za kivita, ambazo vikosi vya Ukraine vinahitaji kwa dharura katika operesheni yake ya kuilinda nchi dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW