Ukraine na Uingereza zatia saini makubaliano ya ushirikiano
10 Aprili 2024Makubaliano hayo yalitiwa saini wakati wa kongamano la kijeshi mjini Kyiv lililohudhuriwa na kampuni 30 za ulinzi za Uingereza.
Baada ya hafla ya kutiwa saini kwa makubaliano hayo, waziri wa viwanda vya kimkakati vya Ukraine Oleksandr Kamyshin, aliwaambia waandishi wa habari kwamba hayo yalikuwa makubaliano ya kwanza ya ushirikiano baina ya serikali.
Shambulizi la droni lashambulia kinu cha nyuklia Ukraine
Kwa upande wake, afisa mkuu mtendaji wa kitengo cha zana za ulinzi na msaada cha Uingereza Andy Start amesema sasa wanatambua kuwa wanahitaji kuimarisha ushirikiano na sekta ya ulinzi ya Ukraine kuiweka katika nafasi bora na kusaidia uchumi wa Ukraine.
Greg Hands, waziri wa sera za kibiashara wa Uingereza, amesema anatumai makubaliano hayo yataleta mafanikio kwa Ukraine katika uwanja wa vita.