Ukraine na Urusi zashambuliana kwa droni na makombora
26 Novemba 2024Jeshi la anga la Ukraine limesema Urusi imefanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani usiku kucha nchini Ukraine na kuharibu majengo na "miundombinu muhimu" katika mikoa kadhaa. Soma: Urusi na Ukraine zashambuliana vikali na droni baada ya mazungumzo ya simu ya Trump na Putin
Jeshi hilo la anga la Ukraine limesema Urusi imerusha droni zilizotengenezwa Iran aina ya Shahed. Jumla ya droni 188 zilirushwa katika mashambulizi hayo.
Jeshi hilo limesema limefanikiwa kudungua ndege 76 za Urusi zisizo na rubani katika mikoa 17, huku zingine 95 zikiwa zimepotea kutoka kwenye rada zao au kuangushwa na mifumo ya kujihami ya kielektroniki.
Moscow na Kyiv zimekuwa zikiongeza mashambulizi ya droni na makombora, huku Ukraine hivi karibuni ikirusha makombora ya masafa marefu ya Marekani dhidi ya Urusi na Kremlin ikilipiza kisasi kwa kutumia kombora la hypersonic.
Moscow pia ilirusha makombora manne ya masafa marefu.