1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Ukraine na Urusi zazima mashambulizi kadhaa ya droni

Saleh Mwanamilongo
24 Novemba 2024

Jeshi la anga la Ukraine limesema limedungua zaidi ya droni 10 za Urusi zilizorushwa kuelekea mji wa Kyiv usiku wa kuamkia Jumapili.

Ukraine na Urusi zazima mashambulizi kadhaa ya ndege zisizo na rubani
Ukraine na Urusi zazima mashambulizi kadhaa ya ndege zisizo na rubaniPicha: U.S. Army/ABACA/picture alliance

Kwa upande wake, Wizara ya Ulinzi ya Urusi iliripoti kuwa zaidi ya droni 30 za Ukraine zilidunguliwa katika ardhi yake usiku wa kuamkia Jumapili.

Mkuu wa mkoa wa Kursk magharibi mwa Urusi amesema droni ishirini na saba na makombora mawili vilirushwa kwenye anga ya mkoa huo na wanajeshi wa Ukraine.

Wakati huohuo, Kampuni ya gesi ya Urusi Gazprom imesema itasafirisha leo Jumapili mita za ujazo milioni 42 za gesi kwenda Ulaya kupitia Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW