1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Urusi na Ukraine zashambuliana kwa makombora

Hawa Bihoga
15 Februari 2024

Urusi na Ukraine zimeendelea kushambuliana leo wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya watu kadhaa ikiwemo watoto na wengine wakijeruhiwa, huku miundombinu muhimu ikiwemo shule, vituo vya nishati na manunuzi vikiharibiwa.

Belgorod, Urusi | Wakaazi wakikagua gari baada ya shambulizi la Ukraine
Wakaazi wa mji wa Belgorod wakikagua gari lao baada ya shambulizi la UkrainePicha: Pavel Kolyadin/ITAR-TASS/IMAGO

 Watu sita wameuwawa mjini Belgorod nchini Urusi akiwemo mtoto mmoja na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio la roketi lililofanywa na Ukraine leo. 

Video zilizosambaaa katika mitandao ya kijamii zinaonesha hali ni tete katika eneo hilo, baadhi ya video zilionesha duka lililoshambuliwa likiwa limeharibiwa vibaya na kuzunguukwa na kifusi, huku mwanamke mmoja akisisika akilia kwa huzuni na baadhi zilionesha mwili uliolalala ardhini ukifunikwa kwa blankenti.

Wizara ya afya ya Urusi imesema katika taarifa yake kwamba kwenye shambulio hilo watu sita wameuwawa akiwemo mtoto mmoja, huku wengine 18 miongoni mwao watoto wanne wakijeruhiwa vibaya. Gavana katika eneo hilo Vyacheslav Gladkov amesema kuwa majengo kadhaa ya makaazi yameharibiwa.

Awali mamlaka katika eneo hilo iliwatahadharisha wakaazi kuongeza umakini baada ya mashambulizi ya vikosi vya Ukraine mwezi Desemba kuuwa watu 25.

Soma pia:Mkuu wa NATO asema kuchelewa msaada wa Marekani kwa Ukraine kunaviumiza vikosi vya Kyiv

Mamia ya watu wakiwemo takriban watoto 400 wameondoka katika mji huo, uhamishwaji mkubwa zaidi nchini Urusi kuwahi kutokea tangu ilipoanzisha uhasama wake dhidi ya Ukraine mnamo Februari 2022.

Wizara ya Ulinzi Urusi imeripoti kudunguwa makombora 14 ya Ukraine katika mji huo wa Belgorod, ambayo yalivurumishwa kwa kutumia mfumo wa kurushia makombora aina ya RM-70 unaoweza kurusha makombora mengi kwa wakati mmoja.

Hata hivyo maafisa wa Urusi hawakusema moja kwa moja ikiwa uharibifu wa majengo ya makaazi ulioripotiwa na mamlaka katika mji huo ulitokana na shambulio la Ukraine au kuangukiwa na majengo.

Urusi yajibu mashambulizi kwenye maeneo ya kimkakati Ukraine

Ndani ya Ukraine kumeshuhudiwa mashambulizi makali, ambapo vikosi vya Urusi vimeendelea kushambulia miundombinu ya muhimu ikiwemo makaazi ya raia.

Mji ya Lviv magharibi mwa Ukraine umeianza siku ya leo kwa mkururo wa makombora yaliyovurumishwa na Urusi na kujeruhi watu kadhaa.

Baadhi ya Waukraine waamua kutoroka kuliko kupigana na Urusi

04:33

This browser does not support the video element.

Mashambulizi hayo pia yanaripotiwa kuharibu vibaya shule, kituo cha nishati na shule ya watoto, huku mashambulizi mengine yakiripotiwa katika mji wa Kharkiv na mji mkuu wa Kyiv.

Mashambulio ya mara kwa mara ya Urusi ya masafa marefu yanatokea huku vita vya takriban miaka miwili vikiwa vimejikita katika makombora na mifumo ya anga yenye uwezo mkubwa zaidi, ambayo inatajwa kuleta uharibifu mkubwa, bila matokeo kwenye uwanja wa vita.

Soma pia:Meli ya Urusi yashambuliwa kwa droni

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ambaye moja ya vipaumbele vyake ni kuboresha mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine, ataingia nchini Ufaransa hapo kesho kutia saini makubaliano ya usalama ya nchi mbili na mwenzake rais Emmanuel Macron kama sehemu ya juhudi zake za kuhakikisha uungaji mkono wa kijeshi wa nchi za Magharibi unaendelea.

Kando na Urafasan Zelensky pia, anatarajiwa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Berlin hapo kesho,wakati wanajeshi wake wakikabiliwa na hali ngumu na uhaba mkubwa silaha ikiwemo risasi na wimbi jipya la mashambulizi ya Urusi.

Hali ngumu kwenye uwanja wa mapambano katika baadhi ya maeneo ya mji wa mashariki wa Avdiivka pia imesababisha Kyiv kuondoa wanajeshi wake, baada ya mapigano kushamiri.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW