1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine: Urusi ina safari ndefu kuikamata Bakhmut

3 Aprili 2023

Ukraine imesema wanajeshi wa Urusi wana safari ndefu sana kuuteka mji wa mashariki wa Bakhmut

Ukraine | Krieg | Kämpfe bei Bachmut
Picha: Cover-Images/IMAGO

Msemaji wa kamandi ya kijeshi ya Ukraine katika eneo hilo, Serhiy Cherevatiy, ameliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu kwamba Bakhmut bado iko chini ya Ukraine na vikosi vya Urusi havijadhibiti chochote na bado wanayo safari ndefu kufikia azma hiyo.

Amesema vita vinaendelea katika maeneo yenye majengo ya kiserikali ambako wapiganaji wa kukodi wa kundi la Wagner wamedai kusimamisha bendera ya Urusi.

Kiongozi wa kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin amesema wanajeshi wake wanaoongoza kampeini ya kuuteka mji wa Bakhmut wameshasimamisha bendera ya Urusi  katika jengo moja la kiutawala katikati ya mji huo, ingawa pia amekiri kwamba wanajeshi wa Ukraine bado wanaukamata mji huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW