1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine: Urusi yadai kusonga mbele katika mji wa Bakhmut

Daniel Gakuba
15 Aprili 2023

Kundi binafsi la wapiganaji la Urusi, Wagner linaripotiwa kuzichukua wilaya mbili mpya katika mji wa Bakhmut mashariki mwa Ukraine

Russland - Ukraine -Krieg I
Picha: Oleksandr Klymenko/REUTERS

Urusi imedai leo kuwa imesonga mbele katika viunga vya kusini na kaskazini vya mji wa Bakhmutmashariki mwa Ukraine, ambao umekuwa uwanja wa mapigano makali kwa miezi kadhaa. Ukraine imesema kuulinda mji huo ni mkakati muhimu wa kuizuia Urusi kulichukua eneo zima la mashariki mwa Ukraine.

Tangazo la wizara ya ulinzi mjini Moscow lililochapishwa leo limesema kuwa wapiganaji wa kundi binafsi la kijeshi la Wagner wamekamata wilaya mbili za mji wa Bakhmut, na kuongeza kuwa vikosi vya Ukraine vinavyorudi nyuma vinaharibu miundombinu na majengo kama mbinu ya kupunguza kasi ya vikosi vya Urusi.

Siku ya Alhamisi Urusi ilisema imewazingira wanajeshi wa Ukraine katika mji huo ulioharibiwa vibaya, lakini Ukraine ilikanusha madai hayo ikisema bado inaweza kuwapelekea wanajeshi wake silaha.

Chanzo: RTRE

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW