1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine yasema imefanya mashambulizi mapya dhidi ya Urusi

16 Agosti 2024

Ukraine siku ya Alhamisi imesema imefanikiwa kufanya mashambulizi mapya dhidi ya Urusi na kuongeza kuwa imekamata zaidi ya kilomita za mraba 1,100,

Kursk | Eneo la Sumy |
Gari ya kijeshi la ukraine likipita karibu na eneo lililoshambuliwa la mpakani katika mkoa wa Sumy, Agosti 14, 2024, katikati ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.Picha: ROMAN PILIPEY/AFP

Ukraine inayashikilia maeneo hayo katika shambulizi kubwa kabisa kufanywa na jeshi la kigeni katika ardhi ya Urusi tangu Vita vya Pili vya Dunia.

Ukraine imesema kwa sasa inadhibiti maeneo kadhaa katika mji wa Sudzha, uliopo kilomita 8 kutokea mpakani.

Jenerali wa ngazi ya juu wa Ukraine aidha amemwambia Rais Volodymyr Zelensky kwamba jeshi limeweka ofisi ya kiutawala kwenye mji huo ili kurejesha sheria na utulivu.

Urusi kwa upande wake imesema imekirejesha kijiji cha kwanza kutoka kilichokamatwa na jeshi la Ukraine katika eneo la mpakani la Kursk na kutangaza kupeleka wanajeshi zaidi kwenye eneo jirani la Belgorod.