SiasaUkraine
Ukraine, Urusi zaripoti vifo baada ya kushambuliana
21 Januari 2026
Matangazo
Raia watatu wametajwa kuuawa kwa mashambulizi ya Urusi katika mji wa kusini mashariki wa Zaporizhzhia nchini Ukraine, kwa mujibu wa Gavana Ivan Fedorov, ambaye alisema mashambulizi hayo yamesababisha pia kukatika kwa umeme kwenye mkoa wake.
Kwa upande wa Urusi, gavana wa mkoa wa Belgorod, ameripoti kifo cha afisa mmoja wa usalama, huku vifo vyengine viwili vikiripotiwa kwenye mkoa wa Bryansk.
Kwengineko, watu wanane wamejeruhiwa kufuatia mripuko katika mji wa Urusi wa Adygea, mashariki mwa Bahari Nyeusi.
Ni nadra kwa Ukraine, ambayo imekuwa ikikabiliana na uvamizi wa Urusi kwa takribani miaka minne sasa, kufanya mashambulizi ndani ya ardhi ya Urusi kutokana na kulemewa kivita.