1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Donetsk: Watu kadhaa wameuawa katika mashambulizi

7 Aprili 2023

Watu kadhaa wameuawa kwenye mashambulizi yaliyoulenga mji wa Donetsk uliopo mashariki mwa Ukraine unaodhibitiwa na Urusi.

Ukraine Krieg | Ukrainische Soldaten im Oblast Donezk
Picha: Muhammed Enes Yildirim/AA/picture alliance

Hadi kufikia hapo jana Alhamisa dadi kamili ya watu waliathirka na mashambulizi hayo haikuwa imethibitishwa. Baadhi ya ripoti za Urusi zinasema watu wanne wameuawa huku nyingine zikitaja kuuawa kwa watu tisa. Kulingana na ripoti za Urusi, shambulizi hilo lililolenga msafara wa magari lilifanywa kwa kutumia makombora ya Marekani aina ya Himars. Video zilionesha magari yalioharibika pamoja na miili kadhaa ya waliokufa. Hata hivyo ripoti hizo hazikuweza kudhibitishwa kwa njia huru. Urusi imeteka rasmi eneo la Donetsk lakini bado inathibiti tu kiasi kidogo zaidi ya nusu ya jimbo hilo . Wakati huo huo mapigano makali yanaendelea katika eneo la Bakhmut lililoko katika jimbo la Donetsk ambapo vikosi vya Ukraine vinaendelea kupinga majaribio ya Urusi ya kuuteka mji huo ambao ulikuwa makazi ya watu 70,000.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW