Ukraine yaahidi mabadiliko ya maafisa wa serikali
24 Januari 2023Hii ni kufuatia kuibuka kwa madai makubwa ya ufisadi tangu Urusi iivamie nchi yake yapata mwaka mmoja uliopita. Polisi ya kupambana na rushwa ilisema Jumapili kuwa ilimkamata naibu waziri wa miundombinu kwa madai ya kupokea hongo ya dola 400,000 kuhusiana na uagizaji wa jenereta kutoka nje ya nchi mwezi Septemba.
Madai ambayo waziri huyo ameyakanusha. Zelensky hakuwataja maafisa walioachishwa kazi. Naibu mkuu wa ofisi ya rais, Kyrylo Tymoshenko, baadae alisema amemuomba Zelensky amuondolee majukumu yake. Hakutoa sababu yoyote lakini vyombo vya habari viliripoti awali kuwa huenda akawa sehemu ya mabadiliko yanayofanywa.
Ripoti za kashfa mpya nchini Ukraine, zinakuja wakati nchi za Umoja wa Ulaya zikibishana kuhusu pendekezo la kuipa Ukraine vifaru vya kisasa aina ya Leopard 2 vinavyotengenezwa na Ujerumani.