1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ukraine yaamuru kuwachiwa wafungwa wa kwanza kutumikia jeshi

23 Mei 2024

Ukraine imeanza kuwaachia wafungwa wa kwanza waliokubali kutumikia jeshi chini ya mpango mpya wa kutoa msamaha kwa walio tayari kupigana vita.

Ukraine | Kvita | Kwapiganaji wa Ukraine
Ukraine inatazamiwa kuandikisha wafungwa wapatao 3,000.Picha: Hanna Sokolova-Stekh/DW

Serikali imesema zaidi wafungwa 3,000 waliomba kujiunga na jeshi tangu kupitishwa kwa sheria inayoidhinishwa kusajiliwa kwao mapema mwezi huu.

Hatua hii inakuja wakati Kyivikikabiliwa na upungufu wa wanajeshi katika uwanja wa vita, na inaakisi mkakati sawa nchini Urusi, ambako makumi ya maelfu ya wafungwa wamepelekwa nchini Ukraine kwa ahadi ya msahama tangu kuanza kwa uvamizi wa Moscow Februari 2022.

Hata hivyo mpango huo hauhusishi wafungwa waliokutwa na hatua ya vurugu za kingono, mauaji ya watu wawili au zaidi, rushwa kubwa na maafisa wa zamani wa ngazi ya juu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW