Ukraine yaangusha maputo ya Urusi kwenye mji mkuu Kyiv
16 Februari 2023Matangazo
Maafisa mjini Kyiv walisema maputo hayo yanaweza kubeba vifaa vya uchunguzi na yalitumwa kupeleleza vikosi vyake vya angani.
Uwepo wa maputo hayo angani ulipelekea ving'ora katika mji mkuu wa Ukraine, jambo ambalo kwa kawaida hutokea wakati makombora yanakaribia.
Soma pia:Ukraine yawaomba washirika wa NATO kuharakisha silaha
Mapema siku hiyo msemaji wa Jeshi la anga la Ukraine, Yuriy Ignat, alisema Urusi inatumia maputo "ambayo hayagharimu chochote" ili kuzima makombora ya kudungulia ndege ya Ukraine.
Tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi mwezi Februari mwaka jana, mamlaka za Ukraine zimeripoti mara kwa mara maputo ya Urusi yanayopeperuka katika anga ya nchi hiyo.