1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yaapa kushinda vita dhidi ya Urusi

24 Februari 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ameadhimisha mwaka wa kwanza wa uvamizi wa Urusi leo Ijumaa kwa kutuma ujumbe mzito wa majonzi kwa watu wake na kusema watashinda kwa kila mtu.

Ukraine | Gedenkveranstaltung zum 1. Jahrestag des russischen Angriffs auf die Ukraine - Wolodymyr Selenskyj
Picha: Ukrainian Presidential Press Office via AP/picture alliance

Katika video iliyotolewa kwa vyombo vya habari iliyopewa jina la "mwaka wa kutoshindwa" akiwa kwenye eneo ambalo alihutubia mwaka mmoja uliopita wakati Urusi ilipoanza mashambulizi yake amesema, wapo tayari, wana nguvu watamshinda kila mtu kama ambavyo walianza mnamo Februari 24, 2022.

Maafisa wa kijeshi wa nchi za Magharibi wanakadiria kuwa pande zote za mzozo huo mkubwa barani Ulaya tangu Vita ya Pili ya Dunia, wanajeshi takribani 100,000 wameuwawa ama kujeruahiwa. Maelfu ya raia wameuwawa huku wengine mamilioni wakilikimbia taifa hilo.

Vikosi vya Ukraine vilizuia ushindi wa mapema mwanzoni mwa 2022, mzozo ambao Urusi unauita  ''operesheni maalum ya kijeshi".