1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yachunguza kuuawa wanajeshi 16

Josephat Charo
2 Oktoba 2024

Ukraine imesema imeanzisha uchunguzi wa kile ilichosema ni kuuwawa kwa wanajeshi wake 16 wafungwa wa kivita kwa kupigwa risasi na vikosi vya Urusi.

Ukraine | Vita vya Urusi
Majeruhi miongoni mwa majeshi ya Ukraine.Picha: Diego Herrera Carcedo/Anadolu/picture alliance

Wanajeshi hao walikuwa wamejisalimisha katika uwanja wa vita mashariki mwa Ukraine.

Mwendesha mashitaka mkuu wa Ukraine, Andry Kostin, amesema hili ni tukio kubwa kuripotiwa la mauaji ya wanajeshi wa Ukraine katika uwanja wa vita na ni ishara nyingine kwamba mauaji na mateso ya wafungwa wa vita si matukio ya nadra.

Soma zaidi: Watu saba wauawa kwa shambulizi la Urusi nchini Ukraine

Kostin alidai hiyo ni sera ya makusudi ya jeshi la Urusi na utawala wake wa kisiasa.

Urusi haikutoa kauli yoyote mara moja kujibu madai hayo.

Utawala wa Kremlin unakanusha kufanya uhalifu wa kivita nchini Ukraine.