1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine yadai kuharibu droni 28 kati ya 31 za Urusi

25 Desemba 2023

Jeshi la Ukraine limesema mfumo wake wa ulinzi wa angani umeharibu droni 28 kati ya 31 pamoja na roketi mbili zilizorushwa na Urusi usiku wa kuamkia leo kuelekea kusini mwa nchi yake.

Vita vya Ukraine | Kherson
Uharibifu ulioyosababishwa na shambulio la Urusi kwenye jengo Kherson.Picha: Ukraine's Kherson Regional Administration/AP/dpa

Kwenye ukurasa wao wa mtandao wa Telegram,jeshi la angani la Ukraine limesema Urusi ilirusha droni hizo kutoka rasi ya Krimea kulenga maeneo ya Odesa, Kherson, Mykolaiv na Donetsk.

Jeshi hilo limesema mabaki ya droni zilizodunguliwa yalianguka na kuharibu vifaa vya kiufundi katika bandari ya Odesa ingawa hakuna yeyote aliyejeruhiwa.

Soa pia: Ukraine yasherehekea Krismasi ya kwanza ya Disemba 25

Hata hivyo, shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha kivyake ripoti hiyo ya Ukraine.

Hapo jana, kila upande kati ya Urusi na Ukraine ulidai kudungua ndege za adui katika maeneo tofauti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW