1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yadai kuharibu meli ya kivita ya Urusi

Sylvia Mwehozi
5 Machi 2024

Ukraine imedai hii leo kuwa imeizamisha meli nyingine ya kivita ya Urusi kwenye Bahari Nyeusi kwa kutumia Droni ya baharini yenye teknolojia ya hali ya juu.

Ujerumani | Mkutano wa Usalama wa Munich | Rais Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akitoa hotuba yake katika Mkutano wa 60 wa Usalama wa Munich (MSC) katika hoteli ya Bayerischer Hof mjini Munich, kusini mwa Ujerumani, Februari 17, 2024.Picha: TOBIAS SCHWARZ/AFP/Getty Images

Taarifa hizo zinatolewa wakati vikosi vya Kiev vikiendelea kuvilenga vikosi vya Urusi kwenye uwanja wa mapambano. Hata hivyo, mamlaka za Urusi hazikuthibitisha madai hayo ya Ukraine.Shirika la kijasusi la jeshi la Ukraine lilisema kitengo cha operesheini maalum kimeharibu meli kubwa ya doria ya Sergey Kotov usiku wa kuamkia leo, kwa kutumia mifumo ya Magura V5 iliyotengenezwa nchini Ukraine na kusheheni milipuko. Meli hiyo ya doria ambayo Ukraine inadai kuwa imeiharibu karibu na mlango bahari wa Kerch, inaripotiwa kuwa na uwezo wa kubeba makombora ya baharini na karibu wafanyakazi 60.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW