1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yadai kuimarisha vikosi vyake huko Bakhmut

9 Januari 2023

Ukraine imesema inaimarisha vikosi vyake huko Bakhmut, mashariki mwa eneo la Donbas na kuzuia mashambulizi ya mara kwa mara ya Urusi yanayofanywa na kundi la mamluki la Urusi la Wagner.

Ukraine-Krieg Bachmut | Russischer Angriff während orthodoxen Weihnachtswaffenruhe
Picha: CLODAGH KILCOYNE/REUTERS

Ukraine imesema inaimarisha vikosi vyake huko Bakhmut, mashariki mwa eneo la Donbas na kuzuia mashambulizi ya mara kwa mara ya Urusi yanayofanywa na kundi la mamluki la Urusi la Wagner. Maafisa wa Ukraine wamesema nchi hiyo ilikuwa imewatuma maafisa zaidi Soledar, mji mdogo karibu na Bakhmut ambapo hali ilikuwa mbaya. Yevgeny Prigozhin ambaye ndiye mwasisi wa kundi hilo la mamluki la Wagner, kwa miezi sasa amejaribu kuiteka Bakhmut na Soledar, jambo lililoshuhudia watu wengi kufariki dunia pande zote mbili. Mbali na hayo, maafisa wa Ukraine wanasema shambulizi la Urusi katika soko kwenye kijiji cha Shevchenkove kilichoko eneo la kaskazini la Kharkiv, limesababisha vifo vya wanawake wawili na kuwajeruhi watu wengine 4 akiwemo msichana mwenye umri wa miaka 10.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW