1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yadai kushambulia mifumo ya kujilinda ya Urusi

30 Oktoba 2023

Ukraine inasema imeshambulia sehemu ya mifumo ya ulinzi wa angani ya Urusi katika eneo la Crimea lililozingirwa a Urusi usiku wa kuamkia Jumatatu.

Maafisa wa Ukraine wamesema Jumatatu mashambulizi ya mabomu na makombora ya Urusi yamesababisha kifo cha mwanamke mmoja na kuwajeruhi watu wengine watano katika maeneo ya Kherson na Odesa.
Maafisa wa Ukraine wamesema Jumatatu mashambulizi ya mabomu na makombora ya Urusi yamesababisha kifo cha mwanamke mmoja na kuwajeruhi watu wengine watano katika maeneo ya Kherson na Odesa.Picha: Anatolii Stepanov/AFP/Getty Images

Haya yamesemwa na kitengo cha mawasiliano ya kimkakati cha jeshi la Ukraine huku Urusi nayo ikisema kuwa imezuia jaribio la shambulizi la kombora katika eneo la Bahari Nyeusi.

Wakati huo huo, maafisa wa Ukraine wamesema Jumatatu mashambulizi ya mabomu na makombora ya Urusi yamesababisha kifo cha mwanamke mmoja na kuwajeruhi watu wengine watano katika maeneo ya Kherson na Odesa.

Roman Mrochko ambaye ni msimamizi wa kijeshi wa mji wa Kherson amesema mwanamke mwenye umri wa miaka 85 ameuwawa kufuatia usiku mzima wa mashambulizi ya Urusi.

Baadae Urusi inaripotiwa kufanya mashambulizi nje ya mji wa Zaporizhzhia ambapo iliharibu miundo msingi ya kijamii.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW