1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ukraine yadai kuzidungua droni 9 kati ya 14 za Urusi

3 Februari 2024

Jeshi la anga la Ukraine limedai kuzidungua hii leo ndege 9 kati ya 14 zisizo na rubani ambazo zimerushwa na Urusi katika mikoa yake ya kati na kusini usiku wa kuamkia leo.

Vita vya Ukraine | Dnipropetrowsk
Uharibifu wa shambulizi la Urusi katika mkoa wa Dnipropetrovsk huko UkrainePicha: State Emergency Service of Ukraine in Dnipropetrovsk region/REUTERS

Jeshi la anga la Ukraine limedai kuzidungua hii leo ndege 9 kati ya 14 zisizo na rubani ambazo zimerushwa na Urusi katika mikoa yake ya kati na kusini usiku wa kuamkia leo.

Soma pia: Shambulizi la droni za Urusi lasababisha raia 40,000 kukosa umeme Ukraine

Kyiv imeongeza kwamba droni nyingi zilikuwa zimeelekezwa kwenye miundombinu ya nishati katika mkoa wa kati wa Dnipropetrovsk ambako maelfu ya watu tayari hawana huduma ya umeme tangu jana Ijumaa.

Mji ulioathirika zaidi ni ule wa Krivyi Rig ambako ndiko anatoka rais Volodymyr Zelensky. Mkuu wa mkoa Sergey Lysak amedai kwamba takribani watu elfu 15,000 wamekatiwa umeme baada ya shambulizi la Droni.

Urusi imekuwa ikiilenga miundombinu ya nishati ya Ukraine wakati wa mashambulizi yake ya takribani miaka miwili na hivyo kusababisha maelfu ya watu kukosa umeme kwa mwaka uliopita.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW