1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yashambulia kambi ya jeshi la anga la Urusi

26 Julai 2024

Ukraine imesema vikosi vyake vimeshambulia kambi ya jeshi la anga ya Urusi katika rasi ya Crimea ambayo imekuwa ikitumika kufanya mashambulizi ya masafa marefu dhidi yake

Ukraine yashambulia kambi ya jeshi la anga la Urusi
Ukraine yashambulia kambi ya jeshi la anga la UrusiPicha: Planet Labs PBC/AP Photo/picture alliance

Katika taarifa, mkuu wa jeshi la Ukraine, amesema uwanja wa ndege wa jeshi hilo katika eneo la Saky, ulioko magharibi mwa Crimea ndio shabaha ya hivi karibuni zaidi kulengwa na kwamba inatathmini matokeo yake.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kwamba eneo hilo la Saky ni moja ya viwanja vya ndege vya jeshi la Urusi vinavyotumika kudhibiti anga, haswa Bahari Nyeusi, na kwa kufanya mashambulizi ya anga katika maeneo ya Ukraine.

Podolyak: Makubaliano na Urusi ni kama 'makubaliano na shetani'

Hata hivyo taarifa hiyo haikusema ni silaha gani iliyotumika. Hakukuwa na tamko la haraka kutoka kwa wizara ya ulinzi ya Urusi ama maafisa wake katika eneo hilo la tukio.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW