Ukraine yafanya mashambulizi nchini Urusi
31 Julai 2026
Matangazo
Gavana wa Volgograd Andrei Bocharov amesema watu watano wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo, huku jengo la makazi na nyumba binafsi zikiharibiwa. Mamlaka za eneo hilo zimeongeza vikosi vya zimamoto kwa ajili ya kukabiliana na moto huo mkubwa. Kyiv inasema mashambulizi hayo yanalenga kuvuruga usambazaji wa mafuta kwa majeshi ya Urusi na kupunguza uwezo wa Moscow kufadhili vita. Ukraine pia imekuwa ikilenga maghala ya Wildberries ikidai kuwa bidhaa za kijeshi zinazotumiwa na wanajeshi wa Urusi huuzwa kupitia jukwaa hilo.