1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yaishutumu Urusi kuwashambulia raia

10 Machi 2023

Rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky amelishutumu jeshi la Urusi kwa kufanya mashambulizi kadhaa ya makombora na ndege zisizo na rubani nchini humo kwa karibu mwezi mmoja.

Ukraine Kiew Luftangriffe durch Russland
Picha: Ruslan Kaniuka/Ukrinform/IMAGO

Zelensky amesema mashambulizi makubwa ya anga mapema jana ni jaribio jengine la serikali ya kigaidi kupigana vita dhidi ya ustaarabu.

Ukraine imesema takribani raia tisa waliuawa wakati wa mashambulizi, yaliyohusisha makombora yaliyorushwa Kiev na kusababisha umeme kukatika katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.  Maafisa wa Ukraine  wamesema watu waliouawa walikuwa wanavijiji katika jimbo la Lviv, karibu na mji wa eneo la mapambano wa Dnieper na mji wa Kharkiv.

Aidha, jeshi la Ukraine limesema limedungua ndege nyingi zisizo na rubani pamoja na makombora wakati wa mashambulizi yaliyofanyika ndani ya mwezi mmoja. hata hivyo, Urusi imeendelea kukanusha madai ya kuwalenga raia katika vita vyake Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW