1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yaituhumu Marekani kuisaidia Urusi

15 Oktoba 2026

Mvutano mpya umeibuka kati ya Ukraine na Marekani baada ya Kyiv kuishutumu Washington kwa kudhoofisha uwezo wake wa kukabiliana na mashambulizi ya Urusi.

Ukraine Kyiv 2026 | Volodymyr Zelenskiy
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine ameituhumu Marekani kwa kushindwa kuisaidia kujibu mashambulizi ya Urusi.Picha: Henry Nicholls/AFP

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema  Marekani  imeshindwa kutoa taarifa za mapema kuhusu makombora ya Urusi yaliyoshambulia nchi hiyo katika siku za karibuni.

Pia ameeleza wasiwasi kuhusu kupungua kwa ufanisi wa mfumo wa mawasiliano ya satelaiti wa Starlink unaotumiwa na jeshi la Ukraine vitani.

Zelensky amemtaka bilionea Elon Musk kusaidia kurejesha huduma hiyo kikamilifu, huku maafisa wa Ukraine wakidai kuwa vikwazo kwenye mfumo huo vimeathiri matumizi ya ndege zisizo na rubani zinazotumika katika operesheni za kijeshi.

Waukraine wakataa wito wa Trump kumchagua rais mpya

01:46

This browser does not support the video element.

Kwa upande wake, Musk amesema maamuzi kuhusu mfumo wa Starshield unaotumiwa na Ukraine hufanywa na serikali ya Marekani na si kampuni yake ya SpaceX.

Matamshi hayo yanakuja baada ya mashambulizi mapya ya Urusi yaliyosababisha vifo vya watu wasiopungua 15 na kuharibu miundombinu ya nishati katika maeneo mbalimbali ya Ukraine, ikiwemo mji mkuu Kyiv.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW