1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yajiandaa kulipiza kisasi kwa kuishambulia Urusi

28 Aprili 2023

Ukraine leo imesema iko tayari kufanya uvamizi kamili wa ardhini kwa ajili ya kuichukua ardhi yake iliyotekwa.

Ukraine Krieg Angriff auf die Stadt Uman
Picha: National Police of Ukraine/AP Photo/picture alliance

Haya yanajiri baada ya Urusi kurusha makombora mapema leo na kusababisha vifo vya karibu watu 21 hilo likiwa shambulizi lake la kwanza kuu katika kipindi cha miezi miwili.

Waziri wa ulinzi wa Ukraine Oleskii Reznikov amewaambia waandishi wa habari kupitia mtandao kwamba, Kyiv inaandaa mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa kutumia mamia ya vifaru na magari ya kijeshi yaliyotumwa na nchi za Magharibi, kwa matuamini ya kuyaondoa majeshi ya Urusi kutoka maeneo inayodai kuyazingira.

Soma pia: Mashambulizi ya Urusi yawaua 12 Ukraine

Vita hivyo vinaelekea hatua muhimu baada ya mashambulizi ya mwezi mzima ya  Urusi katika majira ya baridi, mashambulizi ambayo hayakuwa na manufaa makubwa kwa Urusi licha ya umwagikaji mkubwa wa damu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW