1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yakataa ombi la Putin la kusitisha mapigano kwa muda

Saleh Mwanamilongo
6 Januari 2023

Urusi imesema wanajeshi wa Ukraine wamewashambulia wanajeshi wake leo Ijumaa wakati wa usitishaji mapigano wa saa 36 uliotangazwa kwa upande mmoja na Rais Vladimir Putin.

Urusi yatuma wanajeshi zaidi nchini Belarus huku hofu ya mashambulizi mapya ikiongezeka
Urusi yatuma wanajeshi zaidi nchini Belarus huku hofu ya mashambulizi mapya ikiongezekaPicha: Philipp Schulze/dpa/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema wanajeshi wake wameshambuliwa katika mikoa ya Luhansk, Donetsk na Zaporizhzhia, lakini kwamba wanajeshi wake walikuwa wakizingatia usitishaji huo wa mapigano. Taarifa hiyo inasema makombora manne ya jeshi la Ukraine yalishambulia mji wa Lyman unaoshikiliwa na vikosi vya Urusi.

Shirika la habari la Reuters halikuweza kubaini mara moja ikiwa kulikuwa na utulivu katika uwanja wa mapigano. Serikali ya Kyiv imesema haina nia ya kusitisha mapigano kwa ajili ya pendekezo la kusitisha mapigano la Urusi, ambalo Ukraine na washirika wake wa Magharibi waliita njama iliyoundwa kuipa wakati Moscow wa kuimarisha askari na vifaa.

Igor Konashenkov msemaji wa jeshi la Urusi amesema wataendelea kuheshimu amri ya usitishwaji mapigano.

"Kwa mujibu wa maagizo ya rais wa Shirikisho la Urusi na waziri wa ulinzi wa serikali ya Shirikisho la Urusi, usitishwaji mapigano wa kundi la askari wa Urusi katika eneo la operesheni maalum ya kijeshi ulianza kutoka saa sita kamili za mchana mnamo Januari 6, 2023 hadi saa kumi na mbili asubuhi mnamo Januari 7, 2023 kwenye eneo zima la uwanja wa mapambano nchini Ukraine.''

Ujerumani kupueleka silaha nzito Ukraine

Ujerumani na Marekani kuipatia Ukraine magari ya kivitaPicha: Axel Heimken/dpa/picture alliance

Hii leo kwenye mtandao wake wa kijamii, wizara ya ulinzi ya Ukraine imesema jeshi lake lilishambulia kwa mabomu jeshi ya Urusi kwenye mustari wa mbele wa mapigano katika mji wa Bakhmut.

Taarifa ya wizara hiyo inasema shambulizi hilo ni zawadi ya Krismas (Krismas ya Orthodox) kwa wanajeshi wa Urusi na kuthibitisha kuwa upinzani utaendelea hadi mvamizi wa mwisho wa Urusi atakapoondoka kwenye ardhi ya Ukraine.

Wakati huohuo Ujerumani inapanga kutoa takriban magari 40 ya kijeshi chapa Marder kabla ya mwisho wa mwezi Machi. Makamu wa Kansela, Robert Habeck alisema Berlin inaweza hatimaye kutuma meli zote za silaha zinazofanya kazi.

Tangazo hilo limekuja siku hiyo hiyo ambayo Marekani imeahidi magari ya kivita ya Bradley kwa Ukraine, na siku moja baada ya tangazo kama hilo kutoka Ufaransa. Ujerumani na Marekani pia zimeahidi kuipatia Ukraine mitambo ya kurushia makombora aina ya Patriot.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW