1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yalishambulia kwa makombora eneo la Belgorod

2 Septemba 2024

Vikosi vya Ukraine vimelishambulia eneo la Belgorod katika jitihada za kudhibiri mashambulizi ya Urusi katika himaya yake.

Shambulizi la Ukraine huko Belgorod
Shambulizi la Ukraine huko BelgorodPicha: Belgorod Region Governor Vyacheslav Gladkov Telegram channel/AP/picture alliance

Vikosi vya Ukraine vimelishambulia kwa makombora eneo la Belgorod kusini mwa Urusi na kumuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine kadhaa, wakiwemo watoto wawili ambao walijeruhiwa vibaya.

Taarifa hiyo imetolewa na gavana wa eneo hilo Vyacheslav Gladkov. Galdkov ameandika katika mtandao wake wa Telegram kwamba mtu mmoja alikufa katika kijiji cha Shagarovka karibu na mpaka na Ukraine.

Watu watatu walijeruhiwa huko Shebekino, katika eneo la mpakani, na Gladkov ameripoti mashambulizi katika kijiji kingine angalau kimoja.

Katika shambulizi la awali hapo jana, watu 11 walijeruhiwa, wakiwemo vijana wawili waliofanyiwa upasuaji baada ya kupata majeraha mabaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW