SiasaUkraine
Ukraine yamteua Fedorov kuwa waziri wa ulinzi
14 Januari 2026
Matangazo
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya wabunge 277 kumpigia kura Mykhailo Fedorov kushika wadhifa huo, katika jaribio la pili baada ya kura ya awali kukwama kwa kukosekana kwa wabunge wa kutosha.
Rais Volodymyr Zelensky alikuwa tayari amemteua Fedorov ambaye anatimiza miaka 35 wiki ijayo. Amekuwa waziri wa mageuzi ya kidijitali tangu mwaka 2019 na alisimamia upanuzi wa uzalishaji wa droni baada ya uvamizi wa Urusi mwaka 2022
Wakati huo huo, aliyekuwa waziri wa ulinzi Denys Shmyhal ameteuliwa kuwa waziri wa nishati na naibu waziri mkuu wa kwanza, siku chache baada ya kuondolewa kwenye wizara ya ulinzi, aliyoiongoza kwa chini ya miezi sita.