1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ukraine yaondoa vikosi vyake maeneo ya uwanja wa vita

15 Mei 2024

Ukraine imesema leo vikosi vyake vimerudi nyuma kutoka karibu na vijiji kadhaa mashariki mwa jimbo la Kharkiv, eneo ambalo wanajeshi wa Urusi wanasonga mbele kwa mashambulizi makali tangu wiki iliyopita.

Ukraine | Kharkiv
Uharibifu wa jengo mjini KharkivPicha: Anadolu/picture alliance

Ukraine imesema leo vikosi vyake vimerudi nyuma kutoka karibu na vijiji kadhaa mashariki mwa jimbo la Kharkiv, eneo ambalo wanajeshi wa Urusi wanasonga mbele kwa mashambulizi makali tangu wiki iliyopita.

Jeshi la nchi hiyo limearifu kwamba kwenye baadhi ya maeneo kuzunguka vijiji vya Lukyantsi na Vovchansk limelazimika kuondoa vikosi vyake kwa lengo la kuokoa maisha na uharibifu wa mali.

Hujuma hizo nzito za Urusizimemlazimisha rais Volodomyr Zelensky wa Ukraine kuifuta ziara yake aliyopanga kuifanya leo nchini Uhispania ili kushughulikia hali kwenye uwanja wa mapambano.

Wakati hayo yakijiri waziri mpya wa ulinzi wa Urusi Andrei Belousov amesema kipaumbele cha Moscow hivi sasa kwenye uwanja wa vita ni kupata ushindi huku ikipunguza vifo vya wanajeshi wake. Akizungumza na wabunge siku chache baada ya kuteuliwa na rais Vladimir Putin kumrithi Sergei Shoigu, Belousov amesisitiza kwamba dhamira yake ni kutimiza malengo yote ya kisiasa na kijeshi katika vita vinavyoendelea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW