1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yapambania mpango wa kubadilishana wafungwa na Urusi

16 Novemba 2025

Ukraine imesema inafanya jitihada ili kurejesha mpango wa kubadilishana wafungwa na Urusi, kwa matumaini ya kuachiliwa kwa Waukraine 1,200 wanaoshikiliwa na Urusi.

Ukraine Kiev 2025 | Rais Volodymyr Zelensk
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskPicha: Tetiana Dzhafarova/AFP

 Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema mazungumzo na mikutano kadhaa inaendelea ili kuanzisha upya machakato huo.

Mkuu wa Baraza la Usalama Ukraine, Rustem Umerov, amesema tayari wamefanya mashauriano nchini Uturuki na Umoja wa Falme za Kiarabu kwa msaada wa washirika wa Kyiv.

Ameongeza kuwa pande zote zimekubaliana kurejea makubalianio ya Istanbul ya mwaka 2022, ambayo yaliweka msingi wa kuratibu mpango wa ubadilishanaji wafungwa kwa mpangilio maalum.

Umerov amesema mashauriano zaidi yatafanyika hivi karibuni ili kukamilisha taratibu, akisisitiza kuwa lengo ni Waukraine kurejea nyumbani kusherehekea Krismasi na Mwaka Mpya na familia zao.

Tangu vita kuanza Februari 2022, Ukraine na Urusi wamebadilishana maelfu ya wafungwa, ingawa mara nyingi mpango huo umekwamishwa na mapigano makali yanayoendelea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW