SiasaUkraine
Ukraine yapiga marufuku mtandao wa mawasiliano wa Telegram
21 Septemba 2024Matangazo
Baraza kuu la usalama wa kitaifa mjini Kyiv limesema uamuzi huo umechukuliwa kwa sababu Ukraine inaamini kuwa adui yake Urusi ina uwezo wa kufanya udukuzi na kuchunguza ujumbe unaotumwa kupitia Telegram.
Mkuu wa baraza hilo la usalama wa kitaida Andrey Kovalenko amefahamisha kuwa marufuku hiyo inahusisha vifaa vya mawasiliano vya serikali na wala sio simu binafsi.
Soma pia: Mwanzilishi wa mtandao wa Telegram kufikishwa mahakamani
Mtandao wa Telegram unatumika sana nchini Ukraine na Urusi na umekuwa chanzo muhimu cha kupata habari tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mnamo Februari mwaka 2022.
Hata hivyo maafisa wa usalama wa Ukraine wamekuwa wakielezea wasiwasi wao juu ya usalama wa mtandao huo wa Telegrama hasa wakati wa vita.